.

8/19/2021

Video ya padri akiwabusu wanafunzi wa kike kanisani yachukiza wanamitandao


Picha:screenshot kutoka kwa video.

Padri huyo ambaye anasemekana kuwa wa Kanisa la Anglikana nchini Ghana, anaonyeshwa akiwa amevalia nguo za kijani, kisha aliwaita wanafuniz hao kwenye mimbari, akawavua barakoa zao kabla ya kuwabusu.

Kelele za kushangiliwa pia zinasikika kwenye kanisa hilo.

Kisa hicho kinaripotiwa kutokea katika taasisi ya St Monica’s College of Education, dayosisi ya Asante-Mampong.


 
Uchunguzi wafanywa
Kufuatia kuzagaa kwa video hiyo, uongozi wa Kanisa la Anglikana nchini Ghana, katika taarifa Jumatatu, Agosti 17, umesema kwamba uchunguzi utaanzishwa kufuatia tukio hilo.

Mkuu wa dayosisi hiyo George Dawson-Ahmoah, paia alisema kanisa hilo litashughulikia namna wanafunzi hao watakavyopatiwa ushauri nasaha punde baada ya uchunguzi kukamilika.


"Kanisa limehuzunishwa na habari hizo na lingependa kusema uchunguzi umeanzishwa ghafla na padri huyo atachukuliwa hatua chini ya sheria na kanuni za Kanisa la Anglikana," ilisoma taarifa hiyo.


Padri huyo aliyetambuliwa kwa jina, Obeng Larbi anadaiwa kuwabusu wanafunzi hao wa mwaka wa mwisho kama njia ya kuwashukuru kwa kujitolea kwa kusoma bibilia wakati wa ibada za kanisa hilo

Mpenziwe padri afariki chumbani mwake
Katika tukio tofauti, padri mmoja wa Kanisa Katoliki jijini Lusaka, Zambia, anachunguzwa na polisi baada ya mpenzi wake ambaye ni mke wa wenyewe kuaga dunia chumbani mwake wakati walipokuwa wanafanya ngono.

Abel Mwelwa, anadaiwa kumualika marehemu ambaye jina lake halisi bado halijakuwa wazi, katika makazi yake ya Parokia ya Kanisa Katoliki ya Kaunda Square usiku mtukufu wa Alhamisi.

Kwa mujibu wa ripoti ya LukasaTimes, mwendazake alikuwa amemdanganya mume wake kuwa alikuwa anakwenda kuhudhurua mazishi na kisha kuishia kwa makazi ya padri huyo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger