.

8/11/2021

Waliomburuza Jamaa Kwenye Bodaboda Mpaka Kumuua Wakamatwa

JESHI la Polisi mkoa wa Tanga linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kumshambulia na kumuua mtu mmoja aliyetuhumiwa kuiba pikipiki huko Korogwe.

 

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga amesema marehemu alituhumiwa kuiba pikipiki Korogwe Tanga, Julai 27, mwaka huu na kutokomea nayo kusikojulikana.

 

Baada ya kufanya tukio hilo, Madereva bodaboda wa eneo aliloiba pikipiki hiyo wakaanza kumsaka ambapo baada ya siku chache walimkamata akiwa na pikipiki hiyo.

 

“Baada ya kumkamata walianza kumshambulia kwa vipigo kisha kumfunga kamba kwenye pikipiki na kuanza kumburuza barabarani (barabara ya vumbi). Hata hivyo, kutokana na majeraha makubwa aliyoyapa, mtu huyo alifariki dunia.

 

“Mpaka sasa tumewakamata watu 11 kwa kwa ajili ya uchunguzi na kuhusika na tukio hilo la kinyama. Uchuguzi ukikamilika tutawafikisha mahakamani,” amesema Chatanda.

 

Aidha, RPC Chatanda amewataka wananchi kutojichukulia hatua za kisheria mikononi kwani ni kuvunja sheria, hivyo iwapo kuna uhalifu basi waripoti katika vyombo vya sheria.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger