.

8/22/2021

"Wanaume wa kibongo sitaki mnitongoze" - Shamsa

Ni headlines za staa wa filamu Shamsa Ford ambaye amekataa kutongozwa na wanaume wa kibongo kwa sababu hawana pesa, hawana heshima, wahuni, na waongo.

Shamsa Ford amefunguka hilo kupitia WhatsApp status ambapo ameandika ujumbe ufuatao baada ya kupost picha ya rafiki yake Anita akiwa na mpenzi wake.

"Una bahati Anita, una mwanaume  Billionaire, anakupa unachotaka , anakulea kama malkia, anakupenda na kukuheshimu aisee mshikilie, njoo Bongo tukuhadithie wanaume wetu ukiwaomba pesa wananuna" 

"Yakiwa hayana eti yanasema nakupima, sasa unampima then shida zake ziende wapi, wahuni, waongo, hayana heshima.Wanaume wa kibongo msinitongoze sitaki, itabidi na mimi nivuke Tz nikatafute mwanaume kama wako" ameongeza 

Shamsa Ford kwenye mahusiano yake ya nyuma aliwahi kuwa kwenye ndoa na Chidi Mapenzi pamoja na msanii Nay wa Mitego.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger