.

8/26/2021

Wasanii Kuanza Kulipwa na Vyombo ya Habari Nyimbo zao Zinapochezwa


Katibu Mkuu wa WIzara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema kanuni zinazohusu mirabaha kwa kazi ya sanaa sio kitu kipya kwa vyombo vya habari bali ni sehemu ya utekelezaji wa haki za wasanii na wabunifu wengine kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1999.

Dkt. Abbasi amesema hayo wakati akifungua warsha ya siku moja kwa wadau wa sanaa na habari kuhusu Kanuni za Mirabaha ya wasanii katika vyombo vya habari vya TV, Redio na mitandaoni iliyofanyika Jijini Dar Es Salaam.
-
"Kanuni hizi zikianza utekelezaji Disemba mwaka huu tutaanza kugawa fedha za wasanii ambao watakuwa wamesajili kazi zao COSOTA na pia ambazo zimechezwa kwenye TV, Redio na mitandaoni. Ni kanuni ambazo zinakuja kugeuza kabisa mfumo wa sasa wa nchi yetu kuwa na wasanii na wabunifu maarufu lakini masikini na kuwa na wasanii maarufu lakini matajiri kutokana na ujira unaotokana na ubunifu wao." amesema Dkt. Abbasi.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger