.

8/11/2021

Watu 24 wa familia moja wafariki dunia kwa kula sumu waliodhani ni chumvi

 
Watu 24 wa familia moja wamefariki baada ya kula chakula kinachoshukiwa kuwa na sumu kaskazini magharibi mwa Nigeria. Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Danzanke - katika jimbo la Sokoto.

Kamishna wa Afya wa jimbo Ali Inname aliwaambia waandishi wa habari kwamba familia hiyo ilitumia kimakosa kemikali ya mbolea ambayo ilionekana kama chumvi wakati wa kuandaa chakula siku ya Jumatatu. Alisema wafanyakazi wa afya walijaribu kuokoa maisha ya wahanga bila mafanikio.

Hata hivyo watu wawili wa familia ambao walionja tu chakula hicho sasa wanapata matibabu hospitalini. Kufuatia tukio hilo, maafisa wameshauri tena watu kuweka vitu vyenye sumu mbali na maghala yao ya chakula kwa sababu za usalama.

Matukio kama hayo yanayohusu familia kufa kwa kula sumu yametokea huko Nigeria lakini idadi ya waliokufa katika tukio hili la hivi karibuni ni kubwa sana.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger