Jeshi la Polisi limesema idadi ya Watu waliouwawa na Mtu mwenye Bunduki aliekuwa akifyatua risasi ovyo karibu na Ubalozi wa Ufaransa - Dar es salaam ni Watu wanne ambapo Watatu ni Polisi na mmoja ni Mlinzi wa Kampuni binafsi ya Ulinzi
Tukio limetokea leo, Agosti 25, 2021 katika makutano ya barabara ya Kenyatta na Kinondoni wakati Askari wakiwa kazini alitokea Mtu akawashambulia kwa Bastola na kuchukua Bunduki za Askari hao na kuanza kurusha risasi ovyo
Ukiachia marehemu hao kuna Watu 6 ambao wamejeruhiwa kwenye tukio hili na wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.