.

8/30/2021

Wezi washambulia gari lililobeba chanjo za Kovid-19 na kuiba dozi 300 Wezi washambulia gari lililobeba chanjo za Kovid-19 na kuiba dozi 300
Gari lililobeba aina mpya ya chanjo ya corona (Kovid-19) lilishambuliwa huko Tehran, mji mkuu wa Iran. Ilitangazwa kuwa watu walioshambulia gari hilo waliiba dozi 300 za chanjo.
Gari lililobeba chanjo za corona lilishambuliwa baada ya kutoka kwenye ghala ya Wizara ya Afya ya Iran katika mkoa wa Yaftabad.

Washambuliaji waliiba dozi 300 za chanjo ya Kovid-19, baada ya kumpiga dereva wa gari.

Habari kwamba chanjo hizo ziliibiwa pia zilithibitishwa na Mkuu wa Polisi wa Tehran Husein Rahimi na Meneja Mkuu wa Mahusiano ya Umma wa Wizara ya Afya Kiyanuş Cihanpur.

Mkuu wa Polisi Rahimi alisema kuwa juhudi zinaendelea kuwakamata wezi hao.

 
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger