.

8/24/2021

William Ruto amjibu Uhuru Kenyatta – ''Sitajiuzulu kamwe''
Naibu wa rais nchini Kenya William Ruto siku ya Jumanne alisema kwamba hatojiuzulu saa chache tu baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuwataka wale wasioridhika na serikali yake kuondoka.

Ruto ameapa kusalia katika utawala wa chama cha Jubilee na kwamba hatosalimu amri licha ya wito wa kumtaka ajiuzulu iwapo hakubaliani na ajenda ya rais Uhuru Kenyatta kuliunganisha taifa.

Naibu wa rais amesema kwamba hatotishika na vitisho kutoka kwa maafisa wa serikali aliodai wanafadhaisha kampeni zake kukuza ajenda yake ya uchumi wa Chini kupanda juu {Bottom Up} nchini.

‘’Mimi ni mtu mwenye maono na sina nafasi ya kusalimu amri’’, alisema Dkt William Ruto huko huko Kinango Kwale. Naibu huyo alikuwa akizungumzakatika eneo bunge la kinango kaunti ya Kwale..

Wakati huohuo naibu huyo wa rais alipigia chapuo ajenda yake ya uchumi wa kuimarisha hali ya watu wa chini akisema kwamba alianzisha mazungumzo ambayo Wakenya wengi wamekuwa wakiyakubali.

Alisema kwamba mfumo huo wa uchumi utahakikisha kwamba watu wasio na ajira , wafanyabiashara wadogo wadogo wanaojaribu kujikimu kimaisha wanashirikishwa katika taifa.

Wakati huohuo naibu huyo wa rais amewaambia washindani wake kwamba Kenya sio taifa la watu wachache tu .

‘’Wanafaa kuelewa kwamba mimi ni mtu ambaye siwezi kusalimu amri na nimeamua kubadilisha uchumi kupitia vuguvugu la Hustler na mfumo wa kiuchumi wa ‘Bottom up’.

Aliwashutumu waliowa wakiunga mkono muswada wa BBI kwa kuwa na maslahi ya kibinafsi na ajenda bila kuwajali Wakenya masikini.

‘’Tunataka kujenga taifa ambalo hakuna hata Mkenya mmoja atawachwa nyuma.

Hatutakubali watu wachache kuendeleza maslahi yao ya kibinafsi kwa kubadilisha katiba ili kugawanya nyadhfa bila kuwajali mamilioni ya Wakenya ambao hawana ajira’’, alisema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger