.

8/09/2021

Yanga yatoa sababu ya kuachana na makipa wao
UONGOZI wa Yanga umeeleza kuwa sababu kubwa ya kuachana na nyota zao wawili ambao ni makipa ni kufuata ripoti ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
Ni Metacha Mnata na Faroukh Shikalo ambao wote kandarasi zao zilikuwa zimemeguka na Nabi hakuwa tayari kuona wakiongezewa mkataba.

Kwa mujibu wa Haji Mfikirwa, Kaimu Katibu wa Yanga amesema kuwa ilikuwa ni mapendekezo ya kocha kuachana na wachezaji hao wote wawili.

"Tunafanya kazi kwa kuzingatia ripoti ya mwalimu hivyo ni yeye ambaye alipendekeza tufanye hivyo na hakuna namna nyingine.

"Mnata yeye amepewa barua leo ya kuwa mchezaji huru hivyo tunamtakia kila la kheri pamoja na Shikalo," amesema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger