YouTube yaondoa mamilioni ya video zenye kupotosha kuhusu Corona

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Nembo ya kampuni ya YouTube
Nembo ya kampuni ya YouTube
Mtandao wa Youtube Jumatano umesema umeondoa kwenye mtandao wake zaidi ya video millioni moja za habari hatari za kupotosha kuhusu virusi vya corona, tangu kutokea kwa hilo mwaka iliyopita.

Taarifa ya mtandao huo unaomilikiwa na kampuni ya Google, inajiri wakati mitandao ya kijamii ikishutumiwa vikali na viongozi wa kisiasa kutokana na kushindwa kudhibiti usambazaji wa habari potofu kuhusu virusi vya corona pamoja na mada nyingine.

Youtube imesema katika taarifa kwenye blogi yake kwamba inategemea maelezo ya wataalamu wa afya, ikiwemo kituo cha kudhibiti magonjwa hapa Marekani (CDC) na shirika la afya duniani (WHO), lakini imekuta wakati mwingine kwamba, si rahisi kutambua habari potofu, wakati ukweli mpya unaibuka.

“Sera zetu zinaangazia kuondoa video za aina yoyote ambazo zinaweza kusababisha madhara mabaya kwa ulimwengu,” afisa mkuu anaehusika na bidhaa, Neal Mohan ameandika.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad