.

9/01/2021

Askofu Gwajina Ajipanga Kukiwasha Tena Jumapili?
WAPO wanaosema kuwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima ambaye pia ni mbunge wa Kawe, Jumapili hii huenda akakiwasha tena kanisani kuzungumzia Chanjo kwa vile anatajwa kuwa siyo mtu muoga. Lakini mimi kabla ya yote namuomba asome maandiko haya kwenye Kitabu ta Warumi 13: 1-7.

1 Kila mtu na atii mamlaka inayotawala, kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu, nazo mamlaka zilizopo zimewekwa na Mungu.

Kwa hiyo yeye anayeasi dhidi ya mamlaka inayotawala anaasi dhidi ya kile kilichowekwa na Mungu, nao wale wafanyao hivyo watajiletea hukumu juu yao wenyewe.

Kwa kuwa watawala hawawatishi watu wale wanaotenda mema bali wale wanaotenda mabaya. Je, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Basi tenda lile lililo jema naye atakusifu.

Kwa maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa ajili ya mema. Lakini kama ukitenda mabaya, basi ogopa, kwa kuwa hauinui upanga bila sababu. Yeye ni mtumishi wa Mungu, mjumbe wa Mungu wa kutekeleza adhabu juu ya watenda mabaya.

Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu iwezayo kutolewa, bali pia kwa ajili ya dhamiri.

Kwa sababu hii mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu, ambao hutumia muda wao wote kutawala.

Mlipeni kila mtu kile mnachodaiwa. Kama mnadaiwa kodi lipeni kodi, kama ni ushuru, lipeni ushuru
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

1 comment:

  1. Mamlaka zimewekwa na Mungu na niyingine zimewekwa na wao si Mungu. Acheni kumsingizia Mungu. Hapo ni Shetani 100%. Hawezi kuendeleza huo ujinga wenu. Chanjo ni hiari na mtu anba uhuru wa kusema.Kwa kuwa yupo CCM asiseme kitu. HAPANA. Hakuna mtu wa kuburuzwa hapa. Gwajima nakupa big up. Mimi nipo nyuma yako na wengine wengi sana.

    ReplyDelete

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger