.

9/13/2021

Auawa kwa Kisu Akimzuia Njemba Kufanya Mapenzi na Mhudumu wa Gesti

Mlinzi Kampuni ya Ulinzi ya Mast Holding aitwaye Steven Felician Samandari (25) ameuawa kwa kuchomwa kisu tumboni na mtu aliyekuwa amemkamata baada ya kuruka uzio akifuatilia wahudumu wa Bar/Guest house kwa ajili ya mapenzi Mjini Kahama.

 

Kwa Mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando kwa vyombo vya habari, tukio hilo limetokea Septemba 11,2021 majira ya saa nane usiku katika mtaa wa Nyahanga kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama.

 

“Chanzo cha tukio hilo ni kufuatilia wahudumu wa bar/guest kwa ajili ya mapenzi. Eneo la tukio kimeokotwa kisu kikiwa tumboni. mbinu iliyotumika ni kuchoma kisu tumboni. Mlinzi huyo aliuawa kwa kuchomwa kisu tumboni na mtu aliyekuwa amemkamata baada ya kuruka uzio akifuatilia wahudumu wa bar/guest kwa ajili ya mapenzi,” amesema Kamanda Kyando.

 

Kamanda Kyando amesema Jeshi la Polisi linamshikilia mwanamke aitwaye Fatuma Juma Charles (22), mhudumu wa bar kwa uchunguzi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger