.

9/09/2021

Aunty Ezekiel "Nikisema Nifunguke Mambo Ya Ndani ya Moses Iyobo Patachimbika"STAA wa Tasnia ya Bongo Movie, Aunty Ezekiel amefunguka ya moyoni kumuhusu baba wa mtoto wake ambaye ni mnenguaji wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo akidai kuwa alipotea njia kuingia kwenye mahusiano na kijana huyo.


Ikumbuke tu kuwa wawili hao ambao waliishi pamoja kwa miaka kadhaa na kubahatika kupata mtoto mmoja wa kike, Cookie waliachana na kwa sasa Aunty Ezekiel yupo kwenye mahaba mazito na msanii wa Bongo Bleva, Kussah ambaye tayari wameshapa mtoto huku Iyobo akitajwa kuwa kwenye mahusiano na msanii wa Bongo Fleva, Rubby.


“Kuna mda nafikiliaga juuu ya huyu mwanaume ambaye hajui kuachika, hivi kwenye mahusiano yao sisi tuliingiaje mbona sisi tulikuwa kimya, daaaah muda mwingine najuta kuwai kuwa nae, nikisema nifunguke mambo ya ndani kuhusu yeye kutachafuka,” amesema Aunty Ezekiel.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger