Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Biashara United kucheza bila mashabiki

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limekataa maombi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuruhusu washabiki kwenye mechi kati ya Biashara United na FC Dikhil ya Djibouti.

Mechi hiyo ya marudiano ya Kombe la Shirikisho la CAF itachezwa Jumamosi, Septemba 18 mwaka huu saa 1 kamili jioni Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

CAF imesisitiza kuwa mechi zake zote zitachezwa bila washabiki kama ilivyoainishwa katika mwongozo wake na ule wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuhusu ugonjwa wa Covid-19.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments