Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Chui Aliyevamia Guest House Moshi Alikuwa Kwa Risasi Tatu


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa amethibitisha kuwa chui aliyetoroka katika hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro aliuwawa na Askari wa wanyamapori baada ya kuvamia Zahanati ya Huruma iliyopo Bomang’ombe Hai na kujeruhi watu wanne.

Chui huyo jana aliripotiwa kuvamia maeneo mbalimbali ya makazi ya Watu, Zahanati na hata Guest House moja iliyopo kwenye eneo hilo ambapo RPC Kilimanjaro Simon Maigwa amesema chui huyo ilibidi auwawe kwa kupigwa risasi 3 ili asiendelee kuleta madhara zaidi.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments