Dereva aliyesababisha kifo cha Ngaiza asakwa na Polisi 
​​​​​​​JESHI la Polisi mkoani Kagera linamsaka dereva wa lori lenye namba za usajili T505 CLB aina ya FAW TIPPER aliyefahamika kwa jina moja la Seleman, kwa kusababisha kifo cha mwandishi wa habari wa Azam Media, Nicolaus Ngaiza na kisha kutoroka.

Marehemu Nicolaus Ngaiza enzi za uhai wake.
Kamanda wa Polisi mkoani humo Revocatus Malimi, amesema kuwa uchunguzi wa kina kuhusiana na ajali hiyo iliyotokea jana (Septemba 05, 2021) katika eneo la Gwanseli wilayani Muleba mkoani humo unaendelea.

Malimi amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori hilo kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari na kusababisha kugongana uso kwa uso.

Amewataja waliojeruhiwa kuwa ni dereva wa gari dogo lenye namba za usajili T936 DAE aina ya Nissan Ex- Trail alikokuwa amepanda marehemu Nicolaus aitwaye Terezia Bujiku ambaye pia ni mwanasheria wa shirika la Mhola na mwandishi wa habari wa Clouds Media Group Benson Eustance ambao wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.


gari alilokuwa amepanda marehemu Nicolaus Ngaiza.
"Gari dogo lilikuwa likitoka Wilaya ya Biharamulo kuelekea Bukoba, lori lilikuwa likitoka Bukoba kwenda Kasindaga, yalipofika katika eneo hilo la Gwanseli, lori lilitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kujiridhisha kama kuko salama na ndipo magari hayo yakagongana" amesema RPC Malimi.

Nipashe imefika nyumbani kwa marehemu Nicolaus katika kijiji cha Bwara Bukoba Vijijini na kukuta maandalizi ya kuchimba kaburi  yakiendelea.

Marehemu Nicolaus Ngaiza ameacha mjane na watoto watatu. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, Amina.


💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. So amazing i am little bit ashamed to share this marvelous story about a great Dr Kham who helped me to eradicate my HSV-2, I want to write a little testimony about the good work of doctor Kham who cured me from Hsv 1 and 2 for just 2 week with his herbal medicine, I never believe I can be normal again and have a good life like others I always regretted the day I got diagnose with the virus, I was lost of hope when my doctor told me there is no cure for it but I keep thinking and thinking about my future, if I can have kids of my own well I am so grateful for my helper who get me cured with his herbal medicine, I go online in search of anything that can help me because I can’t deal with it forever so I found this doc Kham email on a blog of someone who was cured by him I quickly contact him for help and explain all my pain to him, he told me not to worry about it there is cure for real, I never believe until he send me the herbal medicine when I order for it and I have it within 4 days that is how I took the medicine for 2 week and the following week I go for test just to confirm I was 100% cured from this sickness what a miracle in my life I am so happy right now, you can also get in contact with him if you have such sickness through dr.khamcaregiver@gmail.com and also WhatsApp him +2348159922297… You can visit his website: https://herbal-dr-kham.jimdosite.com

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad