Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Fahyvanny aanika mazito kuhusu Rayvanny

MWANAMITINDO na mzazi mwenza wa Staa wa Bongofleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Faima Msenga ‘Fahyma au Fahyvanny’ ameweka wazi kuwa hana matatizo na baba wa mtoto wake kwa kuwa anawahudumia vizuri yeye na mwanaye. Anaripoti Matilda Buguye, Dar es Salaam … (endelea).

Mwanamitindo huyo amefunguka hayo leo tarehe 30 Septemba, 2021 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kuhusu ubalozi wa vipodozi kutoka La vista organic product.

Fahyvanny ambaye amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuachana na Rayvanny, amesema anamheshimu sana msanii huyo ambaye ni CEO wa lebo ya Next Level Music.

“Mtoto wetu hakuna anachokikosa kwa sababu kwanza anatuona wote wawili… siwezi kuzungumzia kwa kina zaidi kwa sababu haya ni masuala ya kifamilia,” amesema Fahyma.


 

Aidha, akizungumzia sababu za kutobadilisha jina analolitumia kwenye mtandao wake wa Instagram linalounganisha jina lake na Rayvanny yaani (Fahyvanny), amesema jina hilo limehalalishwa na mtandao huo kwa hiyo ni ngumu kulibadilisha

“Hata kama nikibadilisha jina itakuwa haina maana yeyote kwani nitaonekana mimi nina matatizo, lakini sisi tuko poa na hatuna shida yoyote pia tuna mawasiliano mazuri kama wazazi,” amesema.

Aidha, Mwanamitindo huyo amekanusha sauti zilizozagaa mitandaoni wiki kadhaa zilizopita zikisikika kumuagiza dereva wa bodaboda amfuatilie mpenzi wa sasa wa mzazi mwenzie Rayvanny, Paula ambaye wapo kwenye mahaba mazito.


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments