.

9/03/2021

Fiston Mayele, Awatuliza Mashabiki Yanga

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele, amewatuliza mashabiki wa timu hiyo kwa kutoa kauli nzito iliyoendana namatarajio ya kuipa mafanikio makubwa timu hiyo.

 

Mayele ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo amesajiliwa akitokea AS Vita ya nchini DR Congo.


Mshambuliaji huyo wikiendi iliyopita kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi, alicheza mechi ya kirafiki dhidi ya
Zanaco iliyomalizika kwa Yanga kufungwa 1-2.


Akizungumza na Spoti Xtra, Mayele alisema: “Mashabiki zetu wanatakiwa kuwa wavumilivu kwa sasa kwani ndio kwanza tunaanza, timu bado inaandaliwa vizuri na mwalimu, tunaamini kila kitu kitakuwa sawa.
“Sisi kama wachezaji bado tunaendelea kupambana kwa ajili ya kufanya vizuri msimu ujao.

 

Tunataka kuifikisha timu kwenye malengo. Wasubiri waone.“Hakuna ambaye anapenda kuona timu inafanya vibaya, kama ambavyo mashabiki wanaumia pale matokeo yanavyokuwa mabaya basi na sisi wachezaji tunaumia, hivyo hatutakubali hilo litokee.”


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger