.

9/10/2021

Gari la Marehemu Tupac Shakur lauzwa bilioni 4


Gari la Marehemu Tupac Shakur ambalo alikuwa akilitumia yapata miaka 25 iliyopita aina ya BMW 750IL la mwaka 1996 linauzwa kwa dola milioni 1.7 za Marekani ambazo ni takribani Bilioni 4 za Kitanzania.

Gari hilo ambalo alipigwa nayo risasi akiwa ndani yake usiku wa Septemba 7, mwaka 1996 na kupelekea kufariki dunia siku sita baadaye kufuatia shambulio hilo ambalo liliruhusu risasi nne kuingia mwilini mwake, akiwa na mtayarishaji Suge Knight.

Kwasasa liko kwenye eneo la maonyesho ya magari ya watu maarufu huko Las Vegas limekarabatiwa, mashimo yaliyotokana na risasi yamezibwa na kurudishwa katika hali yake mpya.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger