Hans Pope Kutoka Jela Mpaka Kuwa Bilionea ni Fundisho Kubwa Sana

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA

KAMA NILIVYOTUMIWA: .....Mambos bro. Been reading your review on marehemu kaka yetu Hans Poppe. Marehemu nilikutana naye sana kwenye sekta ya transportation na was always impressed na uwezo wake kwenye sekta kana kwamba alikuwa amesomea sekta hiyo......... Utakumbuka alikuwaga President wa TATOA (Tanzania Truck Owners Association) na pia President wa Transporters Association of Tanzania (TAT) sehemu ambazo zote nilipata nafasi ya ku-engage naye thoroughly kwa maswala yanayohusu transportation in Tanzania lakini pia socially pale Silverpipe Club Kawe ambako alikuwa PATRON mpaka kifo chake:....... Marehemu Hans Poppe alivyotoka jela akaanza kujiingiza kwenye siasa za upinzani na kuingia kwenye chama kimoja cha upinzani. Familia yake wakawa very concerned kwa kuwa walihofia ushiriki wake kwenye siasa za upinzani ukizingatia ndiyo kwanza alikuwa ametoka kwenye kesi ya uhaini utamletea matatizo sana......

Bahati mbaya aling'ang'ania kushiriki kwenye siasa hizo na ikawa tatizo linalosumbua ukoo wake sana. Kaka yake mmoja akafikiri akaona "huyu jamaa atakuwa anajishughulisha na hizi shughuli za siasa labda kwa sababu toka ametoka kifungoni hana shughuli anafanya na labda ana hasira na Serikali". Kwa hiyo huyo kaka yake alichofanya ni kumpa fuel tanker moja (zile fupi) ili afanye biashara ya kusafirisha mafuta kutoka Dar-es-Salaam kwenda mikoani. Marehemu akawa ana-park kwenye vituo vya kuhifadhi mafuta mbalimbali kuvizia tender za kupeleka mafuta mikoani. Hilo tanker alikuwa anaendesha mwenyewe.....,.

Aliacha mambo ya siasa na kufanya kazi hii kwa umakini mkubwa akiwa yeye mwenyewe ndiyo dereva mpaka akafanikiwa kununua fuel tanker nyingine kubwa akahamia kwenye hii gari nyingine kama dereva na nyingine akaajiri dereva.. ...

Akiwa na gari mbili akazidisha juhudi, maarifa na umakini kwenye biashara yake na mara hii alipeleka mafuta nchi jirani pia. Gari mbili zikazaa tatu ; tatu zikazaa nne na zikaendelea kuongezeka mpaka sasa ambako inaaminiwa kuwa ana trucks takribani 200......

Fundisho kubwa tunalolipata kwake ni kuwa wavumilivu na wenyewe nidhamu katika mitikasi yote ambayo tunafanya.....FROM JAIL BIRD TO SUPER BILIONEAZ REST IN PEACE MWAMBA HANSPOPE! END.

Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad