.

9/09/2021

Hatari..Watu 12 Wauawa na Kiboko BwawaniJumla ya watu 12 wameuawa na wanyama aina ya Kiboko katika kipindi cha mwezi Februari 2020 hadi mwezi Agosti mwaka huu katika Bwawa la Mtera wakati wakifanya shughuli za uvuvi kwenye bwawa hilo.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohammed Hassan Moyo, ametoa taarifa hiyo wakati akipokea malalamika kutoka kwa wavuvi wanaovua samaki katika bwawa hilo la Mtera.

Kufuatia hali hiyo baadhi ya wananchi wanaofanya shughuli za uvuvi katika bwawa la hilo wameiomba serikali kuvuna wanyama hao ili kupunguza migongano baina yao na wanyama hao ambao wamekuwa wakihatarisha maisha ya wavuvi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger