.

9/15/2021

Jaji Atoa Dakika za Mapumziko Kesi ya Mbowe
Jaji Mustapha Siyani anayesikiliza kesi ya mbowe na wenzake ametoa dakika 2 kwa ajili ya mapumziko, kuwapa nafasi Mawakili wa upande wa utetezi kupitia hati ya maelezo iliyowasilishwa na Shaidi wa kwanza ACP Ramadhani Kingai.

 

Baadae Mawakili wa utetezi wakaeleza Mahakama kuwa Hati ya Maelezo ina matatizo; kwamba Maelezo yamechukuliwa nje ya muda.

 

Mawakili upande wa utetezi wamewasilisha mapingamizi mawili; #Mosi kuhusu jambo la kisheria, kuahirishwa kwa kesi ya msingi mpaka kuamuliwa kwa pingamizi la pili. Pingamizi la #Pili ni namna ushaidi ulivyopatikana.

 

Jaji amekubaliana na Mawakili wanaomtetea Mbowe na wenzake, juu ya kusitisha usikilizwaji wa kesi ya msingi mpaka mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa utetezi kusikilizwa. Kesi imeahairishwa mpaka leo saa nane mchana, ambapo shauri hilo dogo litasikilizwa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger