Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Joseph Omog akabidhiwa mikoba Mtibwa Sugar
Joseph Omog amekabidhiwa mikoba ya Thiery Hitimana ambaye alipaswa kuwa ndani ya Mtibwa Sugar ya Morogoro na sasa yupo zake Simba.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa tayari kocha huyo amepewa majukumu kuinoa Mtibwa Sugar.

Awali majukumu ya kuinoa Mtibwa Sugar ilibidi yawe mikononi mwa Hitimana ambaye aliletwa Tanzania na timu ya Mtibwa Sugar ila kabla ya kuwaga wino kuinoa timu hiyo mabosi wa Simba wakamvutia kasi na sasa ameshaanza kazi kwenye kikosi hicho.

Kifaru amesema kuwa ni maombi zaidi ya makocha 72 walikuwa nayo mkononi ila wao waliweza kufanya mchujo wao na kufika makocha watano na hatimaye sasa ni Omog atakuwa mbeba mikoba iliyoachwa wazi na Hitimana.

Raia huyo wa Cameroon amewahi kuifundisha Azam FC, AC Leopards pia na Simba hivyo ana uzoefu mkubwa na soka la Tanzania.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments