.

9/04/2021

Kampuni Apple Yasitisha Kukagua Picha zenye Maudhui ya Unyanyasaji wa Kingono kwa Watoto Kwenye Simu za Watumiaji


MAREKANI: Kampuni ya Apple imesema mipango ya Teknolojia yake ya kukagua picha zenye maudhui ya unyanyasaji wa kingono kwa Watoto kwa Watumiaji wa simu za #iPhone imesogezwa mbele

Hatua hiyo imekuja kufuatia ukosoaji mkubwa wa Teknolojia hiyo kutoka Makundi mbalimbali ambayo yaliibua wasiwasi kuwa mfumo huo unaweza kutumiwa vibaya na Serikali zenye mabavu

Katika taarifa yake, #Apple imesema watachukua muda zaidi katika miezi ijayo kufanya mabadiliko kabla ya kuruhusu Teknolojia hiyo ambayo imesisitiza ni muhimu kwa usalama wa Watoto


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger