.

9/11/2021

Kauli ya IGP Sirro baada ya kutua kutoka Rwanda ''tutashirikiana kupambana na ugaidi''


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro, amesema kwa kushirikiana na  Jeshi la Polisi Rwanda, wameazimia kukabiliana na matukio ya kigaidi na hiyo ni kutokana na mkakati waliojiwekea mwezi Mei mwaka huu Jijini Dar es Salaam ambapo utekelezaji wake umeanza.
Kauli hiyo ameitoa alipowasili nchini akitokea nchini Rwanda alipokwenda kwenye ya siku tatu ya kikazi, iliyolenga kuboresha ushirikiano wa kukabiliana na matukio mbalimbali ya kijinai ikiwemo ugaidi.

Pia ameeleza kuwa mkakati mwingine waliojadili ni namna ya kuangalia suala la elimu ya masuala ya kidini inayotolewa kwa watoto wa dini zote kama mafunzo wanayopewa yanalenga kuwapa elimu ya kiroho na kizalendo na si mambo mengine.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger