Kauli ya Manara baada ya Yanga kuchezea kichapo kwa Mkapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA







BAADA ya kikosi cha Yanga kupoteza katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United,  uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kuwa bado una nafasi ya kupata matokeo katika mchezo wa marudio.
Katika mchezo uliochezwa jana Septemba 12, baada ya dakika 90, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 0-1 Yanga jambo lililowapa maumivu mashabiki pamoja na Watanzania kiujumla.

Bao pekee la ushindi lilipachikwa na Moses kwa kichwa akiwa ndani ya 18 baada ya kipa namba moja wa Yanga, Diarra Djigui kutoka kidogo katika eneo lake.

Haji Manara,  Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa kuna dakika 90 za kupambana.

"Tunazo dakika 90 nyingine za kupambania timu yetu, chini ya jua hili hakuna kisichowezekana. Tupeane pole kwa matokeo lakini tusikate tamaa,"

Kibarua kikubwa ni kwenda kushinda mabao zaidi ya mawili kwa sababu wapinzani wao wanafaida ya bao la ugenini.

Mchezo wao wa marudi unatarajiwa kuchezwa Septemba 18 nchini Nigeria na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa hakuna mwenye uhakika wa kusonga mbele kwa wakati huu mpaka dakika hizo 90 zitakapomeguka.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad