.

9/12/2021

Rais Biden afanya ziara katika maeneo yalioshambuliwa kigaidi miaka 20 iliyopita
 Rais wa Marekani Joe Biden ameongoza kumbukumbu ya miaka 20 ya mashambulizi ya kigaidi la Septemba 11 nchini Marekani kwa kufanya ziara katika kila eneo ambalo ndege za kujitoa mhanga zilianguka mnamo mwaka 2001 na kutoa heshima zake kwa wale wote walioathirika kutokana na mkasa huo.
Katika risala yake ya kwanza ya ukimya, Biden alisimama akiwa na huzuni pamoja na waliokuwa marais wa nchi hiyo, Barrack Obama na Bill Clinton, mjini New York City, ambapo shambulio la ndege za kigaidi ziliangusha jengo la maghorofa pacha la Kituo cha Kimataifa cha Biashara. 

Biden hakutoa matamshi yoyote katika eneo lolote la mkasa huo. 

Badala yake, siku ya Ijumaa alitoa video kutuma risala zake kwa wapendwa wa waathiriwa hao, akipongeza umoja wa kitaifa na uzalendo aliosema ulijengeka kutokana na tukio hilo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger