Ticker

6/recent/ticker-posts

Kiongozi wa upinzani afanya mgomo wa chakula Rwanda


Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda anafanya mgomo wa chakula baada ya kukamatwa na polisi, kulingana na wakili wake.
Christopher Kayumba ambaye ni kiongozi wachama cha kisiasa kinachoitwa Rwandese Platform for Democracy (RPD) alikamatwa siku ya Alhamisi kwa mashitaka ya ubakaji, ilisema ofisi ya taifa hilo ya upelelezi (RIB).

Awali Kayumba aliyataka madai dhidi yake ambayo anatuhumiwa kuyafanya katika miaka ya 2012 na 2017, “yenye uchochezi wa kisiasa ”, akidai kuwa yaliibuka siku moja baada ya kuanzisha chama chake mwezi Machi.

Bw Kayumba, ambaye ni mshauri wa masuala ya habari na mhadhiri wa chuo kikuu, alihojiwa kuhusu mashitaka hayo mwezi Machi, na kuitwa kujieleza tena siku ya Alhamisi wili iliyopita ambapo alikamatwa.

Wakili wake Ntirenganya Seif Jean Bosco anasema Bw Kayumba amechukua uamuzi wa kufanya mgomo wa chakula katika mahabusu ya polisi “ili haki yake ya kupewa dhamana iheshimiwe”.

Siku mbili kabla ya kukamatwa kwake, Rais wa Rwanda Paul Kagame alitoa wito wa mfumo wa sheria“kuchukua hatua kali juu ya hususan uhalifu wa ubakaji na unyanyasaji wenye misingi ya jinsia ”

Bw Ntirenganya ameiambia BBC kwamba siku moja kabla ya kukamatwa Bw Kayumba talimwambia kuwa “watu walijtumwa kumuonya akae mbali na siasa vinginevyo atakuwa mashakani ”.

Tangu mwaka huu uanze, Bw Kayumba amekuwa akikosoa sera za serikali za elimu, masharti ya kupambana na Covid, uchumi pamoja na kupelekwa kwa vikosi vya Rwanda nchini Msumbiji.

“Ninahofu kuhudu afya yake sasa kwani amegoma kula chakula. Huo ni uamuzi wa kibinafsi aliouchukuakwa ajili ya haki yake ya kutaka haki yake ya kupewa dhamana iheshimiwe”, anasema Bw Ntirenganya.

Alipokuwa akianzisha chaka chake mwezi Machi, Bw Kayumba alisema kitalenga zaidi katikakile alichokiita “kiong’a Rwanda katika umasikini, kujenga demokrasia ya kudumu na kumaliza dhuluma ”.

 

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments