Kisa Picha ya Paula, Kajala Amwaga Povu

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


VARANGATI limeibuka mtandaoni kufuatia msanii Shebylove kutumia picha inayodaiwa kuwa ni ya mtoto wa Kajala Masanja, Paula wakati akitengeneza cover ya wimbo wake mpya wa #KituKitu bila ridhaa ya mwenye picha ama wazazi wake.

 

Baada ya kuachia cover hiyo, Sheby aliandika maneno haya kupitia ukurasa wake wa Instagram; Kitu kipya hiki #KituKituOUTNOW nimekuekea kwa Chanel yetu usisahau Kusubscribe kulike na kucoment twende YouTube.Jambo hilo limemtibua Kajala ambaye ameonyesha kuchukizwa na kitendo hicho hivyo kumtaka Shebylove aifute picha hiyo haraka vinginevyo atamchukulia hatua za kisheria kwa kutumia picha ya mtoto wake katika matangazo ya cover ya nyimbo yake bila makubaliano.

 

Hata hivyo, Sheby ameonyeshwa kutotishwa na kauli hiyo ambapo amemjibu Kajala kuwa katika cover yake hajatumia picha ya Paula. “Duniani ni wawili wawili.Licha ya hilo, Shabelove pia amemshukuru Kajala kwa ku-subscribe kwenye channel yake hivyo ni shabiki wa kazi zake.

 

Sheby alitupia maneno haya kupitia akaunti yake ya Instagram; Jamani Watanzania na wapenzi wa Mziki wangu ili Swala la Mimi kutishiwa Amani Kisa kazi inayofanya Mimi na Familia Yangu tuishi Eti kisa picture ambayo haijataja mtu Jina Wala kudhihirisha uhalisia Mtoto wa @kajalafrida @therealpaulahkajala inapelekea Mimi kukosa Amani katika Nchi yangu na kazi yangu pia Naomba Jamii tushirikiane katika hili endapo litatokea tatizo lolote basi familia hii itakua chanzo. 

SINA NIA MBAYA LAKINI MANENO YAMENIPA MASWALI MENGI NA KUNIACHA NJIA PANDA!!

 

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad