Ticker

6/recent/ticker-posts

Kumekucha.... Rais Samia "Nani Kawaambia Sigombei 2025?"
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa wapo baadhi ya watu wameanza kumchokoza na kusema kuwa hatagombea urais mwaka 2025.


Rais Samia amesema hayo leo Jumatano, Septemba 15, 2021 wakati akizungumza kwenye kongamano la Siku ya Demokrasia duniani.


“Nataka niwaambie wanawake bado hamjaweka Rais mwanamke, Rais Mwanamke amekaa kwa sababu za kudra za Mungu na Matakwa ya katiba. Sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka madarakani mwaka 2025.


“Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana. Wameanza kuandika andika kwenye vigazeti Samia hagombei, hatasimama 2025 nani kawaambia?


“Fadhila za Mungu zikija mikononi mwako usiziachie. Wanawake tumefanya kazi kubwa sana kuleta uhuru na kujenga siasa za nchi hizi. Tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hizi. Leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani. -Rais Samia Suluhu.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments