Ticker

6/recent/ticker-posts

Kumekucha..Jeshi la Polisi Lamkamata Askari Magereza Kwa Kumbaka na Kumlawiti Binti..Alitaka Kujinyonga Kabla Hajakamatwa


Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala linamshikilia Said Hassan Said (26), Askari Magereza, Mkazi wa Ukonga kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti Msichana mwenye umri wa miaka 29 (jina linahifadhiwa).

“Mnamo Sept 01, 2021 majira ya saa tano nusu usiku katika Barabara ya madafu Ukonga Askrari huyo wa Jeshi la Magereza mwenye namba B 9780 WDR Said Hassan akiwa na mwenzake (bado hajakamatwa) walimkamata kwa nguvu msichana na kumuingiza kwenye gari dogo kisha kuondoka naye hadi kwenye nyumba moja iliyopo karibu na kambi ya KMKM Ukonga Magereza na kuanza kumbaka na kumlawiti kwa zamu” ———-Polisi Ilala

“Baada ya kumaliza kumbaka na kumlawiti Watuhumiwa hao waliendelea kumfanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia na kumsababishia majeraha makubwa na maumivu makali katika sehehmu zake za siri” ———-Polisi Ilala

“Baada ya Mtuhumiwa kugundua kuwa anatafutwa na Polisi kwa tukio baya alilolifanya na mwenzake, mnamo tarehe 02/09/2021
alijaribu kujiua kwa kujinyonga na kuacha ujumbe wa maandishi kwa mkuu wake wa kazi na askari wenzake kuwa———-“mnisamehe bure kwa uamuzi wangu niliochukua kwa tukio nililolifanya nitaonekana nimekufa kizembe” lakini kabla hajafanikisha azma yake ya kujitoa uhai alikamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi”———Polisi Ilala
#MillardAyoUPDATES

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments