Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Kuna Barbara Gonzalez Mmoja tu, Hakika Simba Inang'ara
Huku mjini tunamuita Genius Barbara... Huko kwenu sijui mnamwitaje? Mzuri wa sura mpaka roho yake.. Mchanganyiko wa akili za Kizungu na Kiafrika.. Muite Barbara Gonzalez..
.
Mtendaji Mkuu wa kwanza mwanamke kwenye klabu kubwa ya soka Tanzania.. Mtendaji Mkuu wa kwanza mwanamke kwenye klabu kubwa Afrika Mashariki na kati..Mtendaji Mkuu wa Simba.. Inavutia sana..
.
Kumekuwa na changamoto nyingi tangu kuteuliwa kwake Septemba mwaka jana, lakini ukweli umebaki mbele.. Barbara anajua sana.. Kiongozi shupavu.. Mwanamke Jasiri.. Unajua kwanini? Nitakwambia.

Kumepita Watendaji wengi pale Simba lakini Barbara anabaki kuwa mmoja tu.. Ni mtu wa kipekee.. Ana maamuzi magumu kama mawe ya Mwanza.. Lakini maamuzi yenye manufaa kwa Simba.. Huyo ndio Barbara..

Ana changamoto zake za kawaida kama Mwanadamu.. Ila katika uongozi amejipambanua vilivyo.. #amkanagiftmacha inakuletea maeneo ambayo Barbara ameyaimarisha katika utendaji wake pale Simba..

1. Biashara na Udhamini
Simba ya Barbara inanuka pesa.. Anasaini mikataba ya pesa kila kukicha. Alianza na ule wa Visit Tanzania.. Akaja wa Vunja Bei.. ATCL.. Ule wa Emirates Aluminum kisha ule uliowapa Magari Matatu na Milioni 800 hapo majuzi.. Ni ajabu na kweli. Ni mtendaji gani pale Simba amewahi kuleta mabilioni ya fedha kama haya? HAKUNA... Siyo pale Simba wala Yanga.. Huyu ndio Genius Barbara..

2. Kitengo imara cha Habari na Digital
Nani anaifuatilia Instagram ya Simba? Inapendeza wakati wote.. Kwanza, Barbara alianza kuwekeza kwenye vifaa.. Akawanunulia Rabi Hume na wenzake vifaa vya maana.. Akahakikisha wanasafiri na Simba popote ilipo.. Wakaanzisha Website na App.. Nani alitegemea haya ndani ya muda mfupi? Ni Genius Barbara peke yake..

3. Nidhamu ya Timu
Simba ya sasa imekuwa na Nidhamu kubwa chini ya Barbara.. Nidhamu ya Watendaji wake ipo juu.. Pengine hauko karibu kuyaona haya.. Ila watendaji wa Simba kina Risper, Belinda, George wanafanya kazi kwa weledi mkubwa. Walioshindwa waliondoka ama kuondolewa. Nani amewahi kusikia Mkude akiadhibiwa pale Simba.. Ila wakati wa Barbara yametokea.. Na sasa amekua mtu mwema.

BY Giftmacha

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments