Luis: Simba ni Sababu ya Kufanya Vizuri Al Ahly


KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Simba ambaye sasa amejiunga na mabingwa wa Afrika klabu ya Al Ahly, Luis Miquissone amesema kuwa, ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye kikosi cha wababe hao wa Misri kutokana na uzoefu mkubwa alioupata akiwa nchini Afrika Kusini na ndani ya Simba.

Luis alikamilisha usajili wake na kutangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Al Ahly Agosti 26, mwaka huu akitokea kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba ambayo aliichezea kwa misimu miwili tangu msimu wa 2019/20 na 2020/21.

Akiwa na kikosi cha Simba kwa misimu miwili iliyopita, Luis alifanikiwa kucheza michezo 37 ya Ligi Kuu Bara, na kuhusika katika mabao 25 akifunga mabao 12 na kuasisti mara 13.

Akizungumzia matarajio yake baada ya kujiunga na Al Ahly katika mahojiano maalum Luis alisema: “Kwangu ni jambo kubwa kujiunga na klabu kubwa kama Al Ahly, hii ni ndoto ya kila mchezaji mwenye malengo ya kuwa mchezaji mkubwa, hivyo ilikuwa furaha kwangu kucheza dhidi ya Al Ahly nikiwa na klabu ya Simba kwenye Ligi ya mabingwa Afrika msimu uliopita.

“Nimejifunza mambo mengi nikiwa na Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini lakini pia nikiwa na Simba kwa misimu miwili niliyokuwa Tanzania, naamini kuwa uzoefu nilioupata nikiwa Afrika Kusini na ndani ya Simba utanisaidia kufanya vizuri katika majukumu yangu nikiwa na Al Ahly.”

IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam


______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad