Mama Akutana na Mtoto Wake Baada ya Miaka 58

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Calvin Barrett alikua bila mama yake lakini aliota siku moja kwamba atapatana naye. “Ni kama moyoni mwangu kulikuwa na sehemu tupu hatimaye pamezibwa baada ya miaka yote hii.”



Ndivyo Calvin Barrett anafafanua mwishowe alivyokutana na mama yake baada ya kutengana kwa karibu miaka 60. Barrett mwenye umri wa miaka 64, kutoka Michigan nchini Marekani , alikuwa akimtafuta “Mama yake, Mollie Payne, 88, kutoka Cambridgeshire, kwa karibu miaka 40.


Wawili hao waliunganishwa tena baada ya binti wa Bwana Barrett, Mackenzie Barrett, kufanya uchunguzi wa DNA ambao ulifanana na ya mpwa wake Bi Payne, Stephen Payne.

Bi Payne alikuwa amekutana na mwanajeshi wa angani wa Marekani Bob Barrett mnamo miaka ya 1950 wakati alikuwa huko Uingereza.

lp
Wanandoa hao walioana mnamo Januari 1955 katika Kanisa la St Mary huko Fowlmere, Cambridgeshire, kabla ya kuhamia Marekani mnamo Machi.

Calvin, mtoto wao wa kwanza wa kiume, alizaliwa mnamo 1957 na baada ya mtoto wao wa pili Michael kuzaliwa, Bi Payne alirudi Uingereza.

th
“Nilikuwa na shida nyingi huko Marekani,” anasema. “Wakati huo sikuweza hata kujitunza, sembuse watoto wangu. “Ndugu yangu alinitumia tikiti ya kwenda nyumbani na nilienda na kila nia ya kurudi kwa watoto wangu, lakini hiyo haikutokea.”

Bi Payne alikuwa ametuma barua zilizoandikwa kwa mkono kwa watoto wake, pamoja na zawadi za Krismasi na sanduku za kumbukumbu, lakini wanawe hawakuwahi kuzipokea.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad