.

9/15/2021

Mama atuhumiwa kumuua mtoto wake wa miaka 3 kwa kumkata na shoka

Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia mwanamke aliyefahamika kwa jina la Vaileth Chaula (30) mkazi wa kijiji cha Mkongomi kata ya Kidugala wilayani Wanging'ombe kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kumzaa Azgad (3) kwa kumkata na shoka kichwani na kupelekea kifo chake.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issah amesema kwa mujibu wa maelezo ya wanandugu mwanamke huyo alikuwa na matatizo ya akili.

Alisema miezi michache iliyopita mwanamke huyo akiwa Makambako alipokuwa ameolewa  alipatwa na matatizo ya akili na kurudishwa nyumbani kwao kwa wazazi wake ili apatiwe matibabu.

Alisema akiwa na mtoto huyo ambaye alionekana kudeka, mama yake huyo aliona kuwa anasumbuliwa na mtoto huyo hivyo alichukua shoka ili kumkata kata mtoto huyo.

"Huo ni ukatili tunaita ingawa huyu mama ni mgonjwa lakini sasa sheria haisemi namna hiyo" alisema Issah.

Alisema mwanamke huyo anashikiliwa na jeshi hilo likiwa linasubiri kukamilika kwa baadhi ya mambo ili aweze kufikishwa mahakamani.


 
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger