.

9/10/2021

Mamia wa raia wa kigeni waondoka Afghanistan kwa ndege ya kwanza ya kimataifa


Karibu raia 200 wa kigeni wakiwemo raia wa Marekani wameondoka Afghanistan kwa ndege ya kimataifa kutoka uwanja wa ndege wa Kabul leo. 
 
Hii ndiyo ndege ya kwanza ya abiria kuondoka uwanja huo wa ndege tangu majeshi ya Marekani na nchi zengine za kigeni kukamilisha kuondoka kwao nchini humo mwezi uliopita. 
 
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Qatar iliyoelekea Doha, imeonyesha mafanikio muhimu katika ushirikiano kati ya Marekani na serikali mpya ya Taliban. 
 
Mvutano wa siku nzima kuhusiana na ndege za kibiashara katika uwanja mwengine wa ndege uliwapelekea wasafiri wengi njia panda, jambo lililotilia shaka hakikisho la Taliban la kuwakubalia watu kutoka nchi za nje na Waafghani walio na vibali vya kusafiri kuondoka nchini humo. 
 
Afisa mmoja mwandamizi wa Marekani ambaye hakutaka kutambulishwa, amesema maafisa wawili wa ngazi ya juu wa Taliban ndio waliosaidia kufanikisha safari hiyo.
 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger