Ticker

6/recent/ticker-posts

Manara awaomba radhi Yanga ‘niliteleza’HAJI Sunday Manara, Msemaji wa Mabingwa wa Kihistoria nchini Tanzania, Yanga ya jijini Dar es Salaam amewaomba radhi wanachama na mashabiki wa timu hiyo kwani “kuna mahali niliteleza.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Manara amewaomba radhi juzi Jumanne, tarehe 7 Septemba 2021, alipokaribishwa rasmi makao makuu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es Salaam baada ya kujiunga nao hivi karibuni akitokea kwa watani zao Simba.

Amepokewa na wazee wa timu hiyo ambapo kabla ya kuingia ndani ya ofisi hizo zilizopo mtaa wa Jangwani na Twiga, Manara alinawishwa maji ikiwa ni ishara ya kusafishwa kutoka huko alikokuwa kuingia Yanga.

“Nimerudi kwenye klabu iliyonilea na ya maisha yangu. Wazazi wangu licha ya kucheza na kufanya kazi hapa lakini ndiyo ilinilea.”


 
“Wazee wangu kama kuna mahali lazima niliteleza kiungwana kabisa naombeni msahama wa dhati kabisa. Lazima niliteleza tu na mchukulie kuteleza kwangu ndiyo ilikuwa fursa ya kuja kufanya kazi kwa mabingwa wa kihistoria ‘home of championi,” amesema Manara

Manara amejiunga na Yanga akitokea kwa watani zao Simba nayo ya jijini humo alikoitumikia kama shabiki na msemaji kwa kipindi kirefu na kwa mafanikio makubwa.

Alianza kuzungumza kwa kuwashukuru mashabiki, wanachama na viongozi wa timu hiyo jinsi walivyompokea katika maeneo mbalimbali ikiwemo mitandaoni.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments