Manji "Nilitaka Kumuajiri Hans Poppe Yanga"

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, amemtaja marehemu Zacharia Hans Poppe kuwa ndiye mtu aliyekuwa akimsumbua zaidi enzi zake akiongoza Jangwani.


Manji ameliambia Championi Jumatatu kuwa Hans Poppe ambaye alifariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, ni mtu aliyekuwa ameyatoa maisha yake kwa ajili ya Simba.


Kiongozi huyo amesema yeye binafsi alimheshimu sana Hans Poppe licha ya upinzani waliokuwa nao. “Hans alikuwa ni mpinzani wangu mgumu zaidi katika kazi. Katika namna ya ajabu kabisa, aliyatoa maisha yake kwa ajili ya Simba.


“Kwenye mchezo ule ambao Yanga ilikuwa mbele kwa mabao 3-0, alibadilisha mchezo baada ya nusu saa, naamini yeye ndiye alienda akasema flani atoke na flani aingie na matokeo yakabadilika.


“Nilimheshimu sana. Tulikutana naye kabla ya michezo yote. Alikuwa mtu wa ajabu na akili sana. Kama nisingekuwa mwenyekiti wa Yanga, ningeweza kumuajiri aisaidie Yanga. Alikuwa ‘jiniaz’ (mtu mwenye akili nyingi). Tumempoteza mtu muhimu lakini pia mpinzani wangu mkubwa zaidi.


“Lakini alinifanya mimi na Yanga kuwa bora zaidi, ingawa alikuwa mpinzani. Lakini nilimheshimu sana kama yeye alivyoniheshimu mimi. Alikuwa mtu bora na siyo mbinafsi nafikiri nilikuwa napambana naye kuliko Simba.


“Nifikishieni salamu zangu za rambirambi kwa familia yake. Yanga imempoteza mshindani wao mkubwa,” alisema Manji ambaye alikuwa mwenyekiti wa Yanga kwa miaka mitano tangu 2012 hadi 2017.


Katika kipindi hicho Yanga ilikuwa imetawala soka la Tanzania, huku ikicheza staili maarufu ya pasi ya ‘kampa kampa’ tena na kuanzia Manji ameondoka Yanga hawajatwaa tena kombe la Ligi Kuu Bara.

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad