Mapya yaibuka tukio la daktari aliyefumua mshono wa mgonjwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Dar es Salaam. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesema video inayosambaa mitandaoni ikimuonyesha daktari  aliyemshona jeraha mgonjwa na kufumua mshono  kwa madai ya kushindwa kulipa gharama ni tukio lililotokea Julai,  2021.

Imesema lilitokea  katika kituo cha afya Kerenge kilichopo tarafa ya Magoma halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Ufafanuzi huo umetolewa leo Jumamosi Septemba 4, 2021 baada ya kusambaa kwa video hiyo na kuzua mjadala mtandaoni huku Wizara ya Afya ikitoa tamko na kuomba mwenye kufahamu eneo husika kutoa taarifa na kisha kuweka namba ya simu.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo naibu katibu mkuu Tamisemi anayeshughulikia afya, Dk Grace Magembe amemtaja mtumishi aliyekiuka miiko ya udaktari kuwa ni Dk Jackson Meli ambaye ni ofisa wa kituo hicho cha umma.

“Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo ameshachukua hatua kwa kumsimamisha kazi na amempa hati ya mashtaka na pia ameshafikishwa kwenye baraza la madaktari ili achukuliwe hatua stahiki kwa kwenda kinyume na miiko ya taaluma ya udaktari,” amesema Dk Magembe.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad