google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Mfahamu Kanali Mamady Doumbouya, Kiongozi wa Mapinduzi Nchini Guinea | UDAKU SPECIAL

Mfahamu Kanali Mamady Doumbouya, Kiongozi wa Mapinduzi Nchini Guinea

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Conde, mwenye umri wa miaka 83, alizuiliwa na wanajeshi wa kikosi maalum (GFS) mnamo 5 Septemba, masaa kadhaa baada ya kuripotiwa kwa ufyatulianaji wa risasi karibu na makazi ya rais huko Conakry.


Kamanda wa GFS Kanali Mahamady Doumbouya alithibitisha kuchukua serikali kupitia Runinga ya serikali na kuahidi kusimamia mabadiliko ya serikali kwa njia ya amani



"Ubinafsishaji wa maisha ya kisiasa umekwisha. Tutaweka mpango wa mpito ulio wazi na unaojumuisha watu wote. Tutaweka mfumo ambao [sasa] haupo," Doumbouya alisema wakati akiwa amezungukwa na maafisa wa GFS wenye silaha waliojifunika bendera ya Guinea.



Kanali Doumbouya, ambaye anasemekana alipata mafunzo ya kijeshi nchini Ufaransa, anaonekana kuwa katika uongozi wa kikosi cha jeshi kilichochukua madaraka nchini Guinea kwa jina la National Committee for Rally and Development (CNRD).



"Hali ya kijamii , kisiasa na kiuchumi ya nchi, kutofanya kazi kwa taasisi za jamhuri, udanganyifu wa mfumo wa haki, ukiukaji wa haki za raia, kutokuheshimu kanuni za kidemokrasia, siasa nyingi katika utumishi wa umma, usimamizi mbaya wa kifedha, umasikini na ufisadi umesababisha jeshi la jamhuri kuchukua majukumu yake kwa watu wa Guinea. " 5 Septemba 2021.



"Lazima tusaidie watu wa Guinea kutoka katika hali hii kwa sababu tunaihitaji. Tunamsihi kila mtu akae katika kambi yao na aendelee na shughuli zao za za kawaida ambazo ni pamoja na kulinda mipaka." 5 Septemba 2021.



"Lengo letu ni kuhakikisha kuwa watu wa Guinea wana umoja na wanapata faida zote za nchi. Hatujaja kufanya mzaha na serikali. Tutajifunza kutokana na makosa yote ambayo tumefanya na watu wote wa Guinea. "Kwa France 24, 5 Septemba 2021.



Wanachosema wengine

"Hii inanikumbusha gwaride lililofanyika kwenye Uwanja wa 28 Septemba, ambapo tulihisi kwamba Rais Alpha Conde na Wagini wengine wengine walijivunia kikosi hiki cha vikosi maalum. Ilikuwa, hata hivyo kama mbwa ambaye tulimlisha ambaye aliishia kutushambulia." Mwandishi wa habari kwenye runinga binafsi ya Espace TV, 5 Septemba 2021.



"Huyu hana mafunzo ya kijeshi ambayo yangemruhusu kuwa sajenti katika jeshi la kawaida. Kwa sababu hii, miaka mitano aliyokaa katika jeshi la kigeni huko Ufaransa haikumpeleka zaidi ya hapo ... Kulingana na chanzo chetu, ni vitendo kama hivi, ambavyo ni kusema, kugeuza koplo wa kawaida kuwa kamanda, ambayo inaweza kusababisha wazimu kama huu ambao Koplo Mamady Doumbouya ni mwathirika, ambaye angejitolea kwa mauaji ya watu. " Tovuti ya Le Guepard, 5 Septemba 2021.



"Swali ambalo Wagine wanapaswa kujiuliza ni kama mtu aliyetengwa na jeshi la Ufaransa kwa sababu ya utovu wa nidhamu, na kwa hivyo ni hatari, anaweza kushikilia nafasi ya kamanda katika jeshi la Guinea? Kwa nini lililo baya na hatari katika jeshi la Ufaransa kuwa zuri katika jeshi la Guinea? " Tovuti ya Friaguinee, 23 Agosti 2021.



"WaGinea, ikiwa ungeweza kuepuka kuhadaiwa na mtu atakayekunyonga siku za usoni! Katika siku chache, njiani kuelekea muhula wa tatu wa Alpha Conde, utaelewa ni kwanini aligeuza Koplo Doumbouya kuwa Kamanda Doumbouya." Tovuti ya Le Geupard, 5 Oktoba 2018.



Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (Ecowas), Umoja wa Afrika na UN wamelaani mapinduzi hayo na wanatarajiwa kuweka shinikizo kwa serikali hiyo kukabidhi madaraka kwa serikali ya mpito ya raia.



Mapinduzi nchini Guinea yanaonekana kuchchewa na majibu dhaifu kwa kwa matukio kama hayo katika nchi jirani za Mali na Chad, na kueleza udhaifu wa kisiasa na usalama wa nchi za Afrika magharibi na kati.



Unayofaa kujua kumhusu Doumbouya

Mengi hayajulikana sana juu ya maisha ya utotoni ya Doumbouya, isipokuwa kwamba yeye ni kutoka kabila la Malinke kama Rais Conde na anatoka Mkoa wa Mashariki wa Kankan wa Guinea.



Alikuwa huko Forecariah, magharibi mwa Guinea, ambapo alihudumu chini ya ofisi ya uchunguzi wa eneo (DST) na huduma za ujasusi.



Ana uzoefu wa miaka 15 wa kijeshi ambayo ni pamoja na misheni nchini Afghanistan, Cote d'Ivoire, Djibouti, Jamhuri ya Afrika ya Kati na ulinzi wa watu mashuhuri Israeli, Cyprus , Uingereza na Guinea.



Kanali huyo anasemekana "amekamilisha vyema" mafunzo ya wataalam wa ulinzi wa kiutendaji katika Chuo cha Usalama cha Kimataifa huko Israeli, kozi ya mafunzo ya makamanda wa shule katika Shule ya mafnzo ya kijeshi Senegal, mafunzo ya afisa msimamizi Chuo cha staff College Libreville (EEML) cha Gabon na Chuo cha Vita huko Paris.



Alihudumu kama mwanajeshi wa kigeni yaani 'legionnaire' katika jeshi la Ufaransa hadi 2018 wakati Conde alipomtaka arudi Guinea kuongoza GFS, iliyoanzishwa mwaka huo.



Maisha yenye utata

Tangu 2018, kumekuwa na ripoti kadhaa kwenye vyombo vya habari vya Guinea zikitilia shaka sifa za Doumbouya.



Mnamo Oktoba 2018, Le Guepard aliwaonya watu wa Guinea dhidi ya "kuanguka chini ya ulimi mtamu wa mtu atakayewanyonga siku za usoni".



Mnamo Agosti 2021, Friaguinee lilidai kwamba Dombouya alinyimwa uraia wa Ufaransa kwa sababu "mwenendo wake ulionekana kuwa kinyume na maadili na kanuni" za jeshi la Ufaransa. Ilihoji pia chanzo cha utajiri wa kanali huyo.



Wakati ikiripoti kuhusu mali kadhaa zinazodaiwa kuwa ni za kanali Doumbouya, Friaguinee iliuliza: "Afisa huyu, ambaye anapokea mshahara wa kila mwezi wa chini ya faranga milioni tano [$ 500], anawezaje kujenga majengo haya yote?"



Mnamo Mei, Doumbouya alikuwa miongoni mwa maafisa 25 wa Guinea waliolengwa kwa vikwazo vya EU juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Ni kufuatia uvumi wa kuzuiliwa kwa watu katika Camp Dubreka magharibi mwa Guinea lakini vikwazo hivyo vilifutwa haraka.



Doumbouya pia anaonekana alikuwa akipinga wizara ya ulinzi kusimamia kikosi cha GFS.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad