.

9/10/2021

Mondi, Wema Watajwa Wapenzi Bora Bongo

Kapo ya Miss Tanzania 2006/2007, Wema Isaac Sepetu na staa mkubwa wa muziki nchini Tanzania, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, inatajwa hadi sasa kuwa kapo bora kuwahi kutokea Bongo.

 

Kwa harakaharaka, uchunguzi wa Gazeti la IJUMAA umebaini kwamba, ukizungumizia kipindi cha miaka kumi iliyopita, wapenzi hao wanatajwa kuwa ni wapenzi waliobamba zaidi licha ya kwamba tayari kila mmoja ana maisha yake mengine ya kimapenzi.

 

Mapema wiki hii, Diamond au Mondi aliiibua upya mjadala juu ya penzi lao baada ya kuposti kipande cha video ya wimbo wake mpya wa Naanzaje kisha kusindikiza na ujumbe mrefu uliosomeka;

 

“Nikiitazama hii video, hususan kipande hiki, nakumbuka mbali sana, enzi za mahaba mazito na Madam (Wema), enzi ambazo tulikuwa tunajifungia chumbani wiki nzima, nakwepa kurekodi na hata show ikitokea naitafutia sababu ya kutokuwepo…”Hii ni sehemu ya maneno ya Mondi katika ukurasa wake wa Instagram na kuibua mjadala mzito kwa baadhi ya mashabiki wake.

 

Miongoni mwa watu walioonekana kukumbushwa na kapo hiyo pendwa ni pamoja na mama mzazi wa Mondi, Sanura Kassim au Mama Dangote ambapo alikomenti; “Madam kama Madam Sepeweseeeee…”

 

“Ukatulaza Polisi sababu ya upuuzi wako,” aliandika Moze Iyobo.

“True love never die, hata mgombane vipi, moyo unaongea, haijalishi mpo umbali upi, mmefanyiana mangapi, upo na nani, hatakuja kutokea,” aliandika Esma Platnumz.

 

Baada ya mambo kuzidi kuwa mengi huku baadhi ya watu wakidai kuwa wawili hao wamesharudiana, Gazeti la IJUMAA lilizungumza na Wema ambapo kwa upande wake hakuwa tayari kuzungumza sana, zaidi sana alisema; “No comment…”

 

Lakini mbali na kapo hiyo, Gazeti la IJUMAA linafahamu kwamba, zipo kapo nyingine ambazo nazo zilipendwa zaidi na mashabiki na baadhi zinaendelea kupendwa hadi sasa.

 

VANESSA & JUX

Ukiachana na Wema na Mondi, kapo nyingine iliyowahi kutikisa Bongo na kupendwa zaidi ni pamoja na ile ya Vanessa Mdee au V Money na Jux ambapo kapo yao ilianza kujulikana zaidi mwaka 2015, lakini ni kama Mungu hakupanga wawe pamoja kwani miaka kadhaa baadaye waliachana na sasa Vanessa ni mchumba wa Rotimi na hivi karibuni watajaaliwa mtoto wa kiume.KAJALA & HARMONIZE   

Kajala na Harmonize walikuja kwa mbwembwe nyingi, lakini wakaondoka wapole. Ukisema hukuwahi kuipenda kapo hii utakuwa muongo kwa sababu ni kapo f’lani hivi ambayo ilikuja kuzima kapo zote zilizokuwa zinatikisa kipindi hicho.

 

Kajala na Harmonize walifanya mambo mengi pamoja hadi pale mdudu-mtu alipokuja kuingilia kati na kuwafanya waachane vibaya, tena kwa aibu kubwa.

 

PAULA & RAYVANNY

Licha ya kwamba watu wengi, hasa watu wazima walionekana kutofurahishwa na kapo hii kwa kisingizio kwamba Paula ni mdogo, lakini wala hawakujali kwani waliendelea kusikiliza hisia za mioyo yao na hadi sasa bado wapo pamoja na kuzidi kutikisa mitandaoni kama moto wa kifuu.

 

LULU & MAJIZO

Kiutaniutani walianza uhusiano, mara ghafla watu wakashangaa mrembo Elizabeth Michael ‘Lulu’ amevalishwa pete ya uchumba. Mungu si Athumani, wakafunga ndoa takatifu na sasa wana mtoto wa kiume aitwaye Genesis. Kapo yao inatajwa kuwa miongoni mwa kapo pendwa Bongo.

 

JANJARO & QUEEN LINAH

Huwezi kutaja kapo pendwa Bongo kwa sasa ukaacha kutaja kapo hii. Ni kapo f’lani hivi tulivu na yenye kuonesha upendo wa kweli ndani yake. Ni kapo ambayo imeonekena kupendwa na mashabiki mitandaoni kutokana na aina ya maisha wanayoishi ya upendo mkubwa, kiasi cha kumwagika.

GPL
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger