Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mrembo Mpya wa Mondi Balaa Tupu!

Francia ni mrembo mwenye umri wa miaka 20 aishie na wazazi wake London nchini Uingereza, lakini mwenye asili ya Visiwa vya Madacascar ambaye amezua gumzo kama lote baada ya kupostiwa na staa mkubwa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz.

 

Hivi karibuni, kupitia Insta Story yake, Diamond alimposti ‘kitoto hicho’ akimtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa hivyo kuwafanya wadukuzi kuanza kutafuta pa kuanzia ili kumjua zaidi.

 

Ni kweli mwenyewe anakiri kuwa na umri wa miaka 20 akimzidi Paula Kajala kwa mwaka mmoja.

 

Katika maswali na majibu akiwa Insta Live, baadhi ya Wabongo walipita naye kumuuliza maswali kadha wa kadha.
Miongoni mwa maswali hayo ni kweli kwamba anampenda Diamond? Akajibu ndiyo na ni vizuri kupendana binadamu na binadamu.

 

Anasema siyo yeye tu anayempenda Diamond bali hata mama yake na muda mwingi wanatumia kusikiliza muziki wake.

 

Hata hivyo, kati ya mambo anayojutia ni kutojua Kiswahili na hakuna kitu anachoficha juu yake na Diamond lakini anampenda Diamond na kamwe hawezi kumchukia Diamond kwani ndiye mtu anayempenda pekee hapa duniani.

 

Kubwa kuliko ni madai yake kuwa, bado hajatolewa usichana wake kwani hakuna mahali anapokimbilia kwani ndiyo kwanza ana umri wa miaka 20.

Cc; @sifaelpaul.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments