.

9/11/2021

Msigwa Aanika Meseji Alizochati na Hans Pope Kabla ya Mauti
 

MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ameeleza masikitiko yake kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Zakaria Hans Pope ambaye amefariki dunia jana usiku katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu.

Msigwa amesema mara ya mwisho aliwasiliana na Hans Pope kupitia simu kwa njia ya ujumbe mfupi ambapo alimweleza namna alivyokuwa akiugua na kupatiwa matibabu.

“Nimeshtushwa sana na kifo cha Zacharia HansPope. Tumepoteza mdau muhimu kwa soka la nchi yetu na mtu aliyetamani kuona Tanzania inakaa kwenye viwango vya kimataifa vya soka.


“Poleni sana wanafamilia, uongozi wa Simba SC wachezaji, wapenzi na wanachama wa Simba wapenzi wa soka na wote walioguswa na msiba huu (wa Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya klabu ya Simba, Zakaria Hanspope).

 

“Mara ya mwisho niliwasiliana nae (Hanspope) kwa kuchati nikimpa pole kwa maradhi yanayomkabili, alinijibu huku akiwa kwenye mashine ya oksijeni (mashine ya kumsaidia kupumua). Aliniambia “ugonjwa unatesa sana huu” na baadaye akasisitiza watu wachukue tahadhari.

“Tumuombee (Zakaria Hanspope) apumzike mahali pema, tuwaombee wafiwa na tumuenzi kwa kuendeleza dhamira kubwa aliyekuwa nayo katika kuendeleza soka la Tanzania. Mungu amweke mahali pema peponi, Amina,” amesema MsigwaHABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger