Mtazamo wa Makamba Kuteuliwa Kuwa Waziri

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPAMBUNGE wa Bumbuli kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, (CCM), January Makamba ameteuliwa kuwa Waziri wa Nishati.

 

Enzi za uongozi ya Hayati Rais John Magufuli, Makamba alionekana “mtukutu”, Fasta Julai 2019, akang’olewa Uwaziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

 

Rais Mama Samia Suluhu Hassan juzi alimemteua Makamba kuwa waziri; uteuzi huo wa “mtukutu” una maana gani?

 

Hii inaonyesha kwamba Rais Samia anaiishi imani yake kwamba, yaliyopita si ndwele ya kugangwa ni yajayo na kwamba ukiitwa binadamu makosa ni sehemu yako.

 

Ingawa Makamba na wenzake akiwemo Nape Nnauye walishambuliwa kwa maneno makali wakidaiwa kuwa ni wasaliti na “watukutu” walijtokeza kumuomba radhi Rais Magufuli lakini haikufikiriwa na wengi kwamba wangeweza kupewa uongozi.

 

Kitendo cha Rais Samia kumteua Makamba kimefuta fikra hizo ndiyo maana wengi waliposikia Makamba ‘kaula’ wakasema “heeeh!” Kwa sasa waziri huyo kijana anaongoza kwa kuoga salamu za pongezi mitandaoni.

Richard Manyota NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad