Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mtazamo Wangu Kujiuzulu Kwa Mo Dewji Simba "Mwepesi Kubebwa na Presha za Matokeo"Kuhusu neno KUJIUZULU ni la kawaida duniani kote, mpirani, siasa na hata kwenye mapenzi! Hakuna mgeni kwenye hili

Ramon Calderon aliwahi kujiuzulu Urais wa Real Madrid na kupisha uchaguzi Mkuu uliomleta Perez kwa awamu ya pili na ikumbukwe hata Perez aliwahi pia kujiuzulu

Perez aliwahi kusema kitu kuhusu watu KUJIUZULU, alisema kuna muda mambo hayaendi kisa wewe, kuna muda unajiona nje ya mfumo na kuhitaji mwingine aongoze na kuna muda masherti kadhaa

Well! MO DEWJI wa Simba kajiuzulu Uenyekiti wa klabu ya Simba na majukumu anayo Try Again! Naomba hapa niseme kitu kuhusu MASHERTI

Moja wapo ya matakwa ya FCC ni kuwa huwezi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na bado ukawa Mwekezaji kwenye timu, ni sawa na kusema kesi ya Nyani umpe Ngedere, hapa walitaka kuondoka CONFLICTS OF INTERESTS

Kujiuzulu kwa MO ni dalili za wazi hivi sasa mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa Simba unaenda kutimia rasmi kwakuwa hata FCC walisema mchakato upo mwishoni kukamilika, pongezi kwa MO

Sababu nyingine ya MO kujiuzulu ni kutokana na ratiba yake! Ni ngumu Mwenyekiti kuwa nje ya nchi zaidi ya miezi mitatu hata kama teknolojia imepiga hatua ila Bodi ni shughuli za kila siku

Mambo mengi yalikuwa hayaendi kutokana na kukosekana kwake, hivyo kujiuzulu kwake kunaleta Mwenyekiti ambae atapatikana kwa muda wote na kujihusisha na shughuli zote

FARHAN unasemaje kuhusu MO kujiuzulu? To me ni uamuzi mzuri kwa maslahi ya klabu as long as anasalia kuwa Investor basi hakuna shida, hii pia itasaidia kuondoa presha, MO personally alikuwa mwepesi kubebwa na presha ya matokeo haswa kutweetšŸ˜„ (utani tu)

Hawa wakina Salim wanazijua presha, wanajua kuishi nazo kwakuwa wamezizoea sana

By @jr_farhanjr

#MOROGORO

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments