.

9/10/2021

Mume wa rapa Nicki Minaj Kufungwa Miaka 10 Jela Kisa Kosa la Kijinsia


Mume wa rapa Nicki Minaj, Kenneth "Zoo" Petty '43' amekiri kufanya kosa la kushindwa kujiandikisha kama mtu aliyewahi kufanya makosa ya Ukatili wa kijinsia alivyoanza kuishi ktk jimbo la California kama sheria inavyomtaka afanye.

Baada ya kukiri kosa, Kenneth sasa anasubiri ombi lake kukubaliwa na mahakama huku wakiangalia adhabu atakayotajiwa mnamo Jan 24 2022. Imeripotiwa anaweza kupewa kifungo cha miaka 10 na kuwa chini ya uangalizi ktk maisha yake yote.

Kesi hii inatokana na kosa alilofanya mwaka 1995 la kujaribu kumbaka binti mwenye umri wa miaka 16, alitumikia kifungo cha miaka minne jela na kutoka kwa masharti makali kama kutoa taarifa kwa mamlaka husika kila anapohama jibo lolote nchini Marekani. Kenneth na Nicki Minaj wana mtoto mmoja ktk ndoa yao.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger