Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mwanamuziki Tems Akaribishwa Lebo ya RCA

Staa wa Muziki kutoka nchini Nigeria, Temsbaby amepata shavu kubwa baada ya kusainiwa katika Lebo kubwa ya muziki duniani ya RCARECORD inayomilikiwa na kampuni kubwa ya Sony Music.

Tems ametambulishwa kwenye lebo hiyo kupitia ukarasa rasmi wa lebo hiyo ambao wametupia picha ya msanii huyo na kuandika `Tupo kwenye msimu mpya na kwenye nafasi ya juu mambo yanaendelea kuwa vizuri kwa kuwafikia watu wengi ulimwenguni kote, Temsbaby karibu sana RCA’.

RCA ni moja kati ya lebo kubwa sana za muziki ulimwenguni ambazo zinafanya kazi na wasanii wakubwa duniani kama, Wizkidayo, Chriss Brown, Asaprocky, Aliciakeys, Usher, H.e,r na wasanii wengi duniani.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments