Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mwigizaji Mtunisy Ambaye Aliezaa na Pauline Zongo Awafungukia Mashabiki Waliomkalia KooniMwigizaji @mtunisy ambaye alizaa na Pauline Zongo awafungukia mashabiki waliomkalia kooni kumwambia kakalia u-handsome tu wakati mzazi mwenzie kaharibikiwa

"Wanasema waswahili kuwa muungwana akivuliwa nguo HUCHUTAMA ni sawa na upo MTONI unaoga mara CHIZI kapita na kubeba nguo zako ukimkimbiza ukiwa huna nguo utaonekana wewe ndio CHIZI. Mungu mkubwa ikiwa walio MUHOJI waligundua hayupo sawa na kumpeleka SOBER HOUSE je wewe unaeambiwa ana mtoto nawe jambo ambalo ni kubwa kuliko hata hayo mahojiano UTAMUELEWA tena mtoto keshakuwa mkubwa? Yote tumuachie Mungu na wale wote walio nitusi na kunikashifu NIMEWASAMEHE na bado nitamsaidia huyo mtoto kama mwanadamu mwingine mwenye haki za msingi acha niendelee KUJIHENDSAMNISHA kama nilivyoambiwa AMIN!!!" Ameandika muigizaji huyo maarufu ambaye pia ni mfanyabiashara

@mtunisy na Pauline Zongo waliachana miaka mingi iliyopita ingawa Mtunisy ameelezwa huwa anamhudumia mwanae ambaye kwasasa ni mkubwa

Picha za kulia ni Pauline Zongo wasasa na wa awali kabla ya misukosuko anayopitia sasa akitajwa pia kuathiriwa na madawa ya kulevya

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments