Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Nandy Anasubiria nini Kwa Billnass, Hana Budi Kumuiga Vanessa Mdee

Naweza kufananisha mahusiano ya Nandy na Billnass kama vile ilivyokuwa Jux na Vanessa.
Ukidate na mwanamke ambaye anafanya kazi kama ya yako, siku akipanda cheo wewe ukabaki palepale, wewe kama mwanaume hautojisikia raha kabisa kwasababu sio tamaduni zetu sisi waafrika kuwa na mahusiano na mwanamke aliyekuzidi Cheo, pesa, na wadhifa.

Vanessa mdee mara baada ya kuanza kupiga collabo na wanaigeria tayari ilikuwa ni ishara ya Tahadhari kwa Kaka yetu Jux. Vanessa kapambana sana mpaka akawa msanii mkubwa Tanzania na hata nje ya Tanzania, wakati huo Jux kalala tu, kalizika na mafanikio. Ikafika wakati Vanessa ni Maarufu na mkubwa kimuziki kuliko Jux, hii ikapelekea Jux kuachika na Vanessa akampata Size yake Rotimi.

Upande wa nandy sasa, sijui huyu dada alipewa kipi na billnass, kila mmoja anajua kwamba nandy ni maarufu na mkubwa kimuziki, mafanikio na wadhifa kuliko Billnass, lakini bado anang'ang'ana kama molingo. Nandy inabidi amuache kabisa billnass, Nenga sio size yake, anampwelepweta tu, nandy ni wakudate na kina Diamond, wizkid, davido n.k.

WANAUME TUTAFUTE HELA, LIFE SIO POA.

 Downlaod App ya BLOG Hii Kutoka Google Play Kwa Kubonyeza HAPA>>>

Post a Comment

0 Comments