Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Polisi wa Kenya Afutwa Kazi Akiwa Amepoteza Fahamu kwa Miezi Tisa
Afisa mmoja wa polisi nchini Kenya aliyepotea kazini na kupatikana miezi tisa baadaye kwa sasabu hakuna mtu aliyejua amelazwa hospitali -ameibuka tena.

Reuben Kimutai Lel alitangazwa kutoroka kazi na mshahara wake kusimamishwa baada ya juhudi za wenzake kumtafuta kwa miezi kadhaa kuambulia patupu.

Juhudi zao za kumtafuta kupitia familia yake – ambayo pia ilikua ikimtafuta - hazikufua dafu.

Bw. Kimutai alishtakiwa bila kuwa mahakamani na waranti ya kukamatwa kwake kutolewa. Kesi hiyo baadaye ilifutwa baada ya polisi kushindwa kumpata.

Ilibainika baadaye kwamba afisa huyo alikuwa amelazwa hospitali akiwa amepoteza fahamu – alikuwa ametoweka kutoka Disemba mwaka jana hadi wiki iliyopita alipopata fahamu.

Ijapokuwa hajarudisha kumbukumbu yake kabisa, aliweza kujitambulisha kwa jina na kujieleza alikuwa afisa wa polisi - na mara baada ya hapo shughuli ya kutafuta familia yake ikaanza, kulingana na ripoti ya chombo cha habari nchini humo.

Afisa huyo wa polisi alikuwa mhanga wa ajali ya barabarani iliyotokea jjijini Nairobi, na alilazwa katika hospitali kuu ya rufaa mnamo Disemba 21 kama mtu asiyejulikana. Hakuwa na stakabadhi zozote za kumtambulisha.

Inaripotiwa anatarajiwa kurejeshwa kwenye orodha ya malipo ya huduma ya polisi.


 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments